Jumanne, 14 Machi 2017

: Kamanda Sirro kajibu ombi la Diamond kuhusu biashara ya chips na bodaboda usiku

Baada ya mwimbaji Diamond Platnumz leo march 14 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 ya Clouds TV kuomba serikali iwasaidie vijana wa vibanda vya chipsi pamoja na bodaboda kuhusu ishu ya muda wa kufanya kazi kuanzia saa sita usiku ambapo alisema muda wa usiku chakula hakipatikani na askari wamekuwa wakimwaga vyakula vyao, kamanda kanda maalum Dar es salaam simon Sirro kajibu kuhusu hilo……
>>> “K imsingi askari wetu wanapita kwa ajili ya usalama na kama amevunja sheria kwa kupitiliza muda hapo ni kuchukua chips zake na yeye mwenyewe, lakini kwenye night clubs wana leseni zao na wanamasharti yao na habari nilizopata wanaweza kuendelea mpaka saa 11 kwa hiyo supu, chips zinapatikana kule ndani”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni